MURATHE
Kwa kila mtaa kuna jamaa ambaye ni garagaria, yeye ndie
hupewa all the odd jobs including petty errands, kuosha gari, kufyeka nyasi,
mara ametumwa dukani, kuchota na kupandisha maji kwa gorofa, kupeleka bike za
watoto kwa fundi etc etc, the list is long. The guy is generally not so bright
you can call him a dimwit but he is a darling to everyone as he is very
obedient ata kaa analipwa pesa kidogo, everyone loves him coz si mwizi na pia
wale hawafikishi threshold maybe anawasaidia.
Hapa kwetu mtaani jamaa anaitwa Murathe na anakuaga na
madrama kweli, sijui alitokoka Murarandia pande gani akajipata hapa 001 coz ile
ushamba anakuaga nayo inahitaji maombi ya all televangelists combined, ile kitu
mie humtuma ni Gibleys peke yake saa ile sijiskii kwenda out (na mafegi siku
zile nilikua navuta) after zile vituko amenonyesha. 1) kunasiku nimemtuma
shopping kidogo usiku kwa kiosk anunue kanyama ka soo sukuma mosquito coil na
tissue, jamaa kurudi aliweka kila kitu kwa fridge. 2) siku ingine import
ikamtuma mahamri ya blue asubuhi, jamaa alirudi saa tano after kuzunguka
bamburi yote akitafuta mahamri, kumuuliza why the delay akasema yeye alikua
anaona mahamri za brown peke yake. 3) early one morning kaa ametumwa kongowea
na mama mboga I gave him a lift on the truck na kufika mtopanga posta
nikampatia funguo nanikamwambia number, juu nilikua kwa barabara nikasongeza
gari mbele kidogo, after kindu 3 minutes while I was wondering why the delay
jamaa akaja akaniambia mlango haifunguki ikabidi nipark vizuri nikajifungulie,
weuh, nilipata myamaa kwa main door ya posta akingangana akiishake na fujo
kweli, passersby walikua washaanza kusimama waone ni nini kinachoendelea, bahati
yetu there were no police on patrol tungewekwa ndani na attempted breakin, in
shock nikachukua funguo nanika muonyesha pale masanduku ziko.
Ile kitu ilifanya nimalizane naye kabisa ni ile siku
alinibadilishia puncture, kumbe jamaa hakukaza nut za front left tire, thank
God tire ilitokana kaa bado niko ndai ya estate alafu nut tatu zilikua zimepotea,
I still shudder nikifikilia kaa ingetokana kwa highway ingekuaaje, I had to
borrow nuts from the other tires and from that day ata mech akiguza tire lazima
nizizunguke na spanner tena niconfirm ziko sawa.
Well, you might be wondering why am boring you with hekaya
ya Murathe, jana juu ya ujinga wake karibu afe, saa hii ningekua nampatia
hekaya tofauti. Theres a neighbor of mine mungu amembariki na ameanza kudevelop
kaplot kake, kitu ya kwanza after all the plans na mafundi hua ni kumwaga
materials na mtu huanza na mchanga na mawe, mchanga ya huku hua yatoka Voi au
Malindi and its as fine as beach sand tafauti hua ni rangi tu juu beach sand
iko white, hainaga zile grain kubwa kaa ya ukambani, ata due to the fineness of
the sand nyuma zetu after plaster hua hazipigwi nilo, fundi huvuta steel vizuri
mara kadhaa na hua yatokea poa sana.
Mtu akitaka mchanga bila kupitia broker hua anaenda Malindi
road hapo pirates kugojea lori zikitoka mtoni na hapo ndipo my neighbor alipata
TATA wakaelewana bei. Kufika kwa site Murathe alikua standby kuonyesha
@introvert pale atamwaga mchanga, after kuinua jecki shida ya TATA ikatokea,
mlango ikadinda kufunguka, Jecki ikainuliwa juu kabisa lakini wapi, the door
was stuck, Murathe na ujinga wake akachukua jiwe and banged on the door, hii
mlango ya TATA simnajua hinges yake zinakuaga hapo juu, acha zile lock ziko
chini ziachilie mlango ifunguke na kufumba na kufumbua Murathe
disappeared, Murathe was well and truly
buried under 17 tons of sand.
Quick action by my neighbor na deree and being Sunday most
guys were at home saved the day, manduru zilipigwa and within a minute the area
was a beehive of activity raia ikichimba mchanga na mikono na miguu, Murathe
alifukuliwa after four very long minutes na akakimbizwa kwa Dr. @Luther12 kaa
bado ako na mchanga kwa mapua na mdomo. God is great Murathe hakutuacha lakini
doc alisema kaa angekaa another two minutes he would have been history.
Musiniulize mbisha ziko wapi, mie nimeingia asubuhi ndio
nikapewa story alafu samavicom ikaanza maringo zake, nimetoka kumpa Murathe
pole na ako poa, anasema Mungu alikua anamuita akakataa kuitika.
@Electronics4u ambia watu huko murarandia waje wamchukue
Murathe naona maisha ya Mombasa imemlemea na @introvert muache kudanganya watu
eti TATA ya beba 21 tons.
πππpoor him
ReplyDelete